Kampuni kubwa ya magari nchini Marekani Ford, imetangaza kwamba
itaachana na mpango wake wa kutaka kutengeneza kampuni ya magari nchini
mexico itakayogharimu dola Bilioni 1.6 ili kuwekeza zaidi nchini
Marekani.
Mark Fields ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ford amesema maamuzi
hayo ni matokeo ya kura ya Imani ya wanaounga mkono biashara iliyokuwa
ikiundwa na Donald trump.
Wakati wa kampeni za kuwania kiti cha Urais bwana Trump aliikosoa vikali
kampuni ya Ford kwa kupeleka shughuli za utengezaji wa magari nchini
Mexico na kutishia kuanzisha ushuru kwa magari yatakayotengenezwa nje ya
mipaka na kuuzwa nchini Marekani.
Mapema siku ya jumanne ametoa tishio sawa na hilo kwa kampuni ya General
Motors.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)