WATU 50 wakiwa na watoto wadogo wamenusurika kufa, baada ya kupotea
ndani ya Pori la Akiba la Selous kwa siku saba; huku wakikosa chakula na
maji na kulazimika kula kinyesi cha ng’ombe, damu na mikojo ya
binadamu.
Watu hao ambao ni wafugaji, walikuwa wakihama na mifugo yao
inayokadiriwa kufikia 1,780 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji
mkoani Pwani, yakiwemo Chumvi na Muhoro waliekea Morogoro, ambako
walidai ndiko yalipo makazi yao.
Tukio hilo ambalo si la kawaida kutokea katika pori hilo, lilianzia
Jumatano iliyopita wakati wafugaji hao, walipoanza safari ya kuelekea
Malinyi mkoani Morogoro, wakiongozwa na mwenyeji wao, waliyemtaja kwa
jina la Mzee Mzigua, ambaye hata hivyo wanadai aliwalaghai na
kuwatelekeza.
Wafugaji hao walisema walitembea kwa siku tano ndani ya pori hilo,
wakitarajia kufika Malinyi, yaliko makazi yao. Lakini hali ilikuwa
tofauti, baada ya mwenyeji wao huyo, kuwalaghai kwa kuwapitisha njia
sisizo sahihi.
Walisema waliishiwa chakula na maji ya akiba na mwisho walijikuta
wanatokea ndani ya Pori la Akiba la Selous; huku hali zao zikiwa
zimedhoofu kutokana na njaa na kiu cha maji. Wakiwa safarini, mwenyeji
wao huyo, aliwataka kila mmoja alipe fedha ikiwa ni ujira wake kwa
kuwaonyesha njia. Walidai kuwa walimlipa fedha nyingi.
Wengine walimlipa Sh milioni mbili, Sh milioni moja na wengine Sh
500,000, wakitarajia angewasaidia. Walitembea usiku na mchana ndani ya
pori hilo, wakipishana na wanyama wakali kama simba na nyati, hivyo
kuhatarisha usalama wa maisha yao na watoto wao.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi, baada ya kutimia siku ya tano wakiwa
ndani ya pori hilo, pale walipoishiwa chakula na maji, hivyo kuwalazimu
kuanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu kwaajili ya kukata kiu. Pia
walikula kinyesi chao ili kupunguza njaa. Yule mwenyeji wao
aliwatelekeza baada ya kuona hali zao zimekuwa mbaya.
Alitokomea kusikojulikana, akiwaacha wasijue pa kwenda, hivyo kulazimika
kutelekeza mifugo yao ili kunusuru kwanza maisha yao. Halikadhalika,
wengine walilazimika kunywa mikojo yao na mingine kuwanywesha watoto wao
kunusuru maisha yao, hali iliyowafanya kuathirika kiafya na kushindwa
kuendelea na safari.
Wengine walianguka na kupoteza fahamu. “Sisi tulikuwa tunataka turudi
nyumbani kwetu Morogoro. Huku tulikuja wakati wa operesheni ya Morogoro,
huku tulikuja kununua ng’ombe lakini miji yetu ipo kule Morogoro.
Tukaambatana na huyo mwenyeji wetu aliyejitambulisha kwa jina la Mzee
Mzigua na mtoto wake.
Lakini tunajua mpaka nyumbani kwake”alisema Kiongozi wa msafara wa
wafugaji hao, aliyejitambulisha kwa jina la Lisesi Cherahani Bela na
kuendelea, “Zilitimia kama siku nne tukiwa hatujanywa maji, jua lilikuwa
linawaka, tukaanza kuanguka, tukaanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu,
tulijaribisha kula kinyesi cha ng’ombe, tulikuwa tunakojoa mkojo
tunanywesha hata watoto. Mimi nilikunywa mkojo lita moja, ikaniathiri
hapa kifuani, kumbe mkojo ni kitu kibaya.”
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, kiongozi
huyo alisema baada ya kuona hali inakuwa mbaya zaidi, alitafuta eneo
ambalo lina mtandao wa simu na kufanya mawasiliano na watu mbalimbali,
ambapo alifanikiwa kuwasiliana na watu wa Kigoma na kuomba msaada wao.
Alisema kuwa watu hao, waliwasiliana na wahifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi na kuwasiliana na wahifadhi wa Pori hilo la Selous, ambao
walianza kazi ya kuwasaka na hatimaye kuwakuta katika eneo la Mlima
Luhombelo, lililopo katikati ya Pori hilo wakiwa tayari wameshadhoofika
kiafya.
Askari hao wa wanyamapori wa Pori hilo, waliwapatia uji na maji na
kuwapa huduma ya kwanza wale wengine ambao walikuwa na hali mbaya.
Baada ya taarifa hizo za kupotea kwa wafugaji hao, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Gaudence Milanzi alifika katika eneo hilo juzi,
akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania
(TAWA), Martin Leibooki, Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock
Msocha na maofisa wengine wa wizara na pori hilo.
Milanzi alisema Serikali inaangalia namna ya kuwasaidia wafugaji hao,
kurejea katika hali zao kiafya pamoja na kuwasaidia kutafuta mifugo yao
ili waweze kurejea katika makazi yao na kuendelea na shughuli zao.
“Kwa upande wa Serikali kama Wizara hatuchukulii kama hawa wameingia
kwenye hifadhi hapana, muhimu kwanza ni kuokoa maisha ya binadamu, na
hicho ndicho tunategemea kukifanya sasa hivi, na baada ya hapo kutakuwa
na masuala ya kutafuta hiyo mifugo, kwa sababu wamepata hasara
kubwa”alisema Katibu Mkuu huyo.
Aliutaka uongozi wa wilaya ya Rufiji, kutoa ushirikiano na wizara ili
kuwabaini waliowadanganya wafugaji hao, kwa kuwaingiza kwenye pori hilo
na kuwatapeli kiasi hicho kikubwa cha fedha.
“Hawa waliowadanganya na kupita huko ndani ya pori kwa kweli tutaendelea
kuwatafuta na tutaomba tuwe na ushirikiano na uongozi wa Wilaya kwa
sababu inaelekea kuna watu kazi yao ndo hiyo, ukiangalia pesa walizowapa
ni nyingi sana, sasa watu wamechukua pesa zote na wamewaacha katika
hali kama hii, wengine wana watoto wadogo, kwa hiyo tutahakikisha
tunashirikiana kuwatafuta ili tukomeshe hili tatizo moja kwa
moja”alisema.
Katibu Mkuu huyo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA na Mhifadhi Selous
kwa juhudi za haraka walizochukua. Alisema wizara yake itaendelea
kushirikiana na Mamlaka mbalimbali, kutoa misaada ya haraka, endapo
yatatokea tena matukio ya aina hiyo.
Kwa upande wake, Leibooki alisema TAWA ambao ndiyo wamiliki wa hifadhi
zote za wanyamapori nchini, haitawachukulia hatua za kisheria wafugaji
hao, kwa kuwa waliingia ndani ya pori kwa kudanganywa na watu wenye nia
mbaya.
Lakini, alisisitiza kuwa mamlaka yake, itawashughulikia kisheria
wawindaji haramu na wafugaji wanaoingiza mifugo yao ndani ya hifadhi
zilizo chini ya Mamlaka yake.
Pia alisema Mamlaka yake, inaendelea na utaratibu wa kushirikiana na
wananchi waishio pembezeni mwa hifadhi zote, kwa kuwapa elimu ya ufugaji
bora kwa kushirikiana na wizara zinazohusika na kuendeleza miradi ya
maendeleo, ikiwemo miundombinu ya maji.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji chini (CCWT), Magembe Makoye aliwataka
viongozi wa Halmashauri mbalimbali nchini, kutatua migogoro ya wakulima
na wafugaji mahali walipo, bila ya kuondoa watu wengine.
Alisema kuwa wao kama chama, wamesikitishwa na tukio la kuondolewa kwa
wafugaji hao katika bonde hilo la Rufiji, kwa kuwaambia warudi
walipotoka. Alisema tamko hilo lilitolewa na uongozi wa Halmashauri hiyo
na ndilo lililosababisha matatizo hayo.
Makoye alisema kufanya hivyo, hakuondoi migogoro ya wafugaji na
wakulima, badala yake ni kuendelea kuzalisha migogoro hiyo katika maeneo
mengine, ambayo wafugaji watahamia.
“Tunalaani kweli vitendo hivi vya viongozi na watendaji wengine wa
Halmashauri kuwafukuza wafugaji, tena wakati mwingine kwa kuwatisha na
matokeo yake wananchi hawa 50 wangepoteza maisha, kama isingekuwa bahati
ya mtu mmoja kuwa na simu kati yao” alisema Katibu Mkuu huyo.
“Kwa kweli kwa niaba ya wafugaji wote wa Tanzania naishukuru sana Wizara
ya Maliasili kupitia kwa Katibu Mkuu, Gaudence Milanzi.” alisema Katibu
huyo.
Alisema kuwa kungeweza kutokea majanga makubwa zaidi kwa kuwa kuwa
wafugaji hao walikuwa wakisafiri na watoto wao wadogo katika mazingira
hatarishi katikati ya pori hilo, ambalo lina wanyama wakali.
“Kwa kweli ni mazingira ya kusikitisha. Lakini niishukuru sana Serikali
kwa maana ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wamefanya kazi yao kwa namna
ambavyo mimi ninawiwa kuwashukuru. Tangu jana tumewasiliana na Katibu
Mkuu wa Wizara, leo watu wote wameweza kupatikana, kumefanyika doria ya
ndege, doria za magari, doria kwa miguu, wamewatafuta hawa watu,
wamewaokoa, wamewaleta kwenye huduma za afya, wamewapa chakula,
wamewahifadhi, hawajawadhuru”
alisema.
Aliiomba Serikali kuhakikisha tatizo la wafugaji nchini, linatafutiwa
ufumbuzi wa kudumu, kwani jamii haiwezi kuendelea kubaki na tatizo hilo
kwa miaka yote. Alitaka wafugaji watafutiwe maeneo ya kudumu ya kufugia,
ikiwa ni pamoja na kupimiwa maeneo yao, badala ya hali ilivyo sasa
kuafukuza kila kukicha.
www.domdaily14.blogspot.com
Friday, 6 January 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Blog Archive
-
▼
2017
(61)
- ► March 2017 (3)
- ► February 2017 (12)
-
▼
January 2017
(46)
- Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Nne na mtihani wa ...
- Gazeti lapewa saa 24 kumuomba radhi Rais Magufuli
- Ugomvi wa DC, Mbunge wa CCM wamfikia Waziri Mkuu
- Faru Fausta wa Ngorongoro atimiza Miaka 54, Aishi ...
- Haya hapa Mambo matano kwenye Taarifa ya kwanza ya...
- Mwanafunzi Chuo cha Ardhi Dar kizimbani kwa Kuchap...
- Siku 118 toka aufunge uwanja wa Taifa Waziri Nape ...
- Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA ...
- PICHA: Rais Barrow alivyowasili Gambia
- Watu 14 akiwemo raia wa China wahofiwa kufa Mgodini
- Tetesi Kuhusu Adebayor kutua Yanga,..isome hii ya ...
- Faini yamgeukia Trafiki Dar es Salaam, aagizwa na ...
- Trump Kaanza Kuwatimua Watu Marekani.......Tayari ...
- Trump Kuzuia wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu Afr...
- Kauli ya Tundu Lissu baada ya chaguzi ndogo kumali...
- Donald Trump kawafuta kazi Mabalozi wote wa Mareka...
- Waziri Anjela Kairuki aiaga Dar leo na Kuhamia Dodoma
- PICHA: Magari ya Kifahari ya Rais Jammeh Yaliyozui...
- Profesa Lipumba Anusurika Kipigo kutoka kwa Vijana...
- Maiti iliyozikwa na Baadae Kukutwa Iko Nyumbani Ki...
- Wizara zote zatakiwa Kuhamia Dodoma kabla ya Feb. 28
- Haya Hapa Magazeti ya Leo Ijumaa January 20
- Sababu za Edward Lowassa Kukamatwa na Polisi Jana
- Hii Hapa Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Baada Ya ...
- Ndege ya Mizigo Yaanguka na Kugonga Nyumba za Watu...
- Hivi ndivyo vipigo vitakatifu alivyowahi kupata Pe...
- Lugha ya Asili Yawachanganya Walimu Dodoma.....Wak...
- Haya hapa Magazeti ya Leo Ijumaa January 13
- Mmiliki wa gazeti la Lete Mambo Atupwa Selo..........
- Mazito Yazidi Kuibuka Anglikana........Askofu Moki...
- Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa ...
- Uteuzi wa Trump Waibua Maswali
- TALGWU Yakemea Watumishi wa Serikali za Mitaa Kudh...
- PICHA: Muonekano wa sasa wa Jennifer na Patrick 'W...
- Hii ndo Nchi ya Kwanza Duniani Kuzima Mitambo ya R...
- Lowassa, Maalim Seif Wawasha Moto Zanzibar
- PICHA: BILLICANAS YA MBOWE YAANZA KUBOMOLEWA RASMI
- Kafulila Kukabidhiwa Kadi ya CHADEMA Jimboni Kwake.
- Kitoweo cha samaki chaondoa uhai wa mtu
- Bosi mpya Tanesco kuwadhibiti 'vishoka'
- 50 wanusurika kufa ndani ya pori la Akiba.
- Trump asababisha Ford kusitisha kutengenezea magar...
- MOI yaelemewa na majeruhi wa ajali
- RC aomba sheria ya kutembea na sime ifutwe
- HALI YA STAA MWINGINE BONGO BAADA YA MATUMIZI YA D...
- Akwepa 'MAWE' kabla ya kuchomwa 'MKUKI' mdomoni
-
►
2016
(1)
- ► December 2016 (1)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)