www.domdaily14.blogspot.com
Wednesday, 4 January 2017
MOI yaelemewa na majeruhi wa ajali
TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) imeishauri Serikali kuongeza
uwezo katika hospitali zake za mkoa jijini Dar es Salaam, ama kujenga
taasisi nyingine kama hiyo nne.
Hatua hiyo itapunguza msongamano wa majeruhi wa ajali wanaotibiwa hapo,
ambao kwa siku ni wagonjwa 30.
Pia serikali imeshauriwa kuijengea taasisi hiyo utaalam wa kuelimisha
wataalam zaidi katika kuhudumia majeruhi wa ubongo, uti wa mgongo,
mishipa ya fahamu na viungo vikubwa kama nyonga na magoti.
Mkurugenzi wa Tiba wa MOI, Dk. Samuel Swai alitoa ushauri huo jana
alipozungumza na Habari-Leo kuhusu wastani wa majeruhi wanaopokelewa kwa
siku katika taasisi hiyo.
Dk Swai alisema kati ya wastani wa wagonjwa 30 wanaowapata kwa siku, 20
hadi 25 wanahitaji upasuaji.
Kati ya hao, walioumia vichwa ndani ya ubongo ni watano hadi 10,
waliobaki wameumia sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo mifupa mirefu,
mikono, miguu, mifupa ya paja na nyonga.
Alisema walioumia migongo ni kati ya wawili hadi watatu, mmoja wao
anaweza akawa amepoteza mawasiliano kwenye mikono na miguu au miguu peke
yake.
“Kati ya majeruhi hao wa bodaboda ni 10 hadi 15, kati ya hao wameumia
sana maeneo ya vichwa, migongo na miguu,” alisema Dk. Swai.
Akizungumzia watoto wanaofikishwa hapo, wengi wao wamevunjika viwiko,
mguu wa paja au mikono.
“Sisi tunaamini wanaopata ajali ni wengi lakini wanaofikishwa hapa ni
wale walioumia sana, wengine wanatibiwa huko huko kwenye hospitali za
mkoa kama Hospitali teuli ya Tumbi, Mwananyamala na nyinginezo,”
alisema.
Alisema hapo Moi wana meza mbili za upasuaji wa majeruhi kwa saa 24,
lakini kuna siku wanapokea wagonjwa kati ya 60 hadi 100 kama kuna ajali
ya basi.
“Kwa kuwa majeruhi wanakuwa wengi zaidi inatubidi wafunge meza za
kawaida ziweze kuhudumia majeruhi” alisema.
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Blog Archive
-
▼
2017
(61)
- ► March 2017 (3)
- ► February 2017 (12)
-
▼
January 2017
(46)
- Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Nne na mtihani wa ...
- Gazeti lapewa saa 24 kumuomba radhi Rais Magufuli
- Ugomvi wa DC, Mbunge wa CCM wamfikia Waziri Mkuu
- Faru Fausta wa Ngorongoro atimiza Miaka 54, Aishi ...
- Haya hapa Mambo matano kwenye Taarifa ya kwanza ya...
- Mwanafunzi Chuo cha Ardhi Dar kizimbani kwa Kuchap...
- Siku 118 toka aufunge uwanja wa Taifa Waziri Nape ...
- Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA ...
- PICHA: Rais Barrow alivyowasili Gambia
- Watu 14 akiwemo raia wa China wahofiwa kufa Mgodini
- Tetesi Kuhusu Adebayor kutua Yanga,..isome hii ya ...
- Faini yamgeukia Trafiki Dar es Salaam, aagizwa na ...
- Trump Kaanza Kuwatimua Watu Marekani.......Tayari ...
- Trump Kuzuia wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu Afr...
- Kauli ya Tundu Lissu baada ya chaguzi ndogo kumali...
- Donald Trump kawafuta kazi Mabalozi wote wa Mareka...
- Waziri Anjela Kairuki aiaga Dar leo na Kuhamia Dodoma
- PICHA: Magari ya Kifahari ya Rais Jammeh Yaliyozui...
- Profesa Lipumba Anusurika Kipigo kutoka kwa Vijana...
- Maiti iliyozikwa na Baadae Kukutwa Iko Nyumbani Ki...
- Wizara zote zatakiwa Kuhamia Dodoma kabla ya Feb. 28
- Haya Hapa Magazeti ya Leo Ijumaa January 20
- Sababu za Edward Lowassa Kukamatwa na Polisi Jana
- Hii Hapa Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Baada Ya ...
- Ndege ya Mizigo Yaanguka na Kugonga Nyumba za Watu...
- Hivi ndivyo vipigo vitakatifu alivyowahi kupata Pe...
- Lugha ya Asili Yawachanganya Walimu Dodoma.....Wak...
- Haya hapa Magazeti ya Leo Ijumaa January 13
- Mmiliki wa gazeti la Lete Mambo Atupwa Selo..........
- Mazito Yazidi Kuibuka Anglikana........Askofu Moki...
- Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa ...
- Uteuzi wa Trump Waibua Maswali
- TALGWU Yakemea Watumishi wa Serikali za Mitaa Kudh...
- PICHA: Muonekano wa sasa wa Jennifer na Patrick 'W...
- Hii ndo Nchi ya Kwanza Duniani Kuzima Mitambo ya R...
- Lowassa, Maalim Seif Wawasha Moto Zanzibar
- PICHA: BILLICANAS YA MBOWE YAANZA KUBOMOLEWA RASMI
- Kafulila Kukabidhiwa Kadi ya CHADEMA Jimboni Kwake.
- Kitoweo cha samaki chaondoa uhai wa mtu
- Bosi mpya Tanesco kuwadhibiti 'vishoka'
- 50 wanusurika kufa ndani ya pori la Akiba.
- Trump asababisha Ford kusitisha kutengenezea magar...
- MOI yaelemewa na majeruhi wa ajali
- RC aomba sheria ya kutembea na sime ifutwe
- HALI YA STAA MWINGINE BONGO BAADA YA MATUMIZI YA D...
- Akwepa 'MAWE' kabla ya kuchomwa 'MKUKI' mdomoni
-
►
2016
(1)
- ► December 2016 (1)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)