Mkazi
mmoja wa kijiji cha Kalundi kilichopo kata ya Kipande wilayani Nkasi,
Vedast Kazumba (51) amejiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa
alighadhabika, baada ya mkewe kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo.
Alisema
ni la usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya na kwamba Kazumba alifikia uamuzi
huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani .
Alieleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo na uchunguzi wake unaendelea .
Habari
kutoka kijijini humo, zinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni
kukasirishwa na kitendo cha mkewe, Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha
samaki mbichi.
“Mke
wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha
usiku, kitoweo chake kikiwa ni samaki mbichi alimkomba samaki huyo kisha
akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha samaki, lakini mkewe
alimweleza kuwa kitoweo hicho kimekwisha. Ndipo mumewe alipokasirika
akidai kuwa mkewe amemnyima kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua
hatua ya kuzira kula“ alieleza mmoja wa mashuhuda kwa masharti ya kutoandikwa.
Akizungumzia
mkasa huo , Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalundi , John Kalasa alidai kuwa
marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na ghadhabu
ambapo mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)