www.domdaily14.blogspot.com

Wednesday, 22 March 2017

Ripoti ya Makonda kuivamia Clouds yakabidhiwa kwa Waziri Nape Nnauye

Ni siku kadhaa zimepita tangu tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia Clouds Media akiwa na askari wenye silaha ambapo ilifuatiwa na Waziri mwenye dhamana ya Habari, Nape Moses Nnauye kutembelea Clouds na kuunda Kamati ambayo ingechunguza ishu hiyo. Sasa leo March 22 2017 Kamati hiyo imetoa matokeo ya uchunguzi huo.

Kamati imesema;
'waliitwa ofisi ya mkuu wa mkoa na kuelekezwa ngazi za kutumia, lakini mkuu wa mkoa alitumia ngazi nyingine kutoka ofisini kwake na kuwatoroka.'

Amesema 'Makonda aliingia kwenye studio ambazo hakutakiwa kuingia, kamati imethibitisha kulikuwa na vitisho ikiwemo kushika silaha za moto na kuwatishia kuwafunga jela miezi sita'.

'Pia aliwatishia wafanyakazi Clouds kuwa angewafunga miezi 6 pia angewaingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya'. 

'Alitoa vitisho kwa wafanyakazi waliokuwa zamu na kusisitiza iwapo wangesema kilichotokea, wangejua yeye ni nani'.

'Ni kweli kwamba Makonda ana kawaida ya kwenda Clouds, mgeni mwenyeji. Ameshawahi kukaa wakati wa kuandaa kipindi chake cha mwaka mmoja mpaka saa 10 alfajiri'.

'Kamati haikuona uthibitisho wa wafanyakazi kupigwa au kukatwa mitama isipokuwa waliolia walitishiwa kwenda jela miezi sita bila kupitia mahakama'.

'Paul Makonda anatakiwa kuomba radhi, Waziri Nape Nnauye awasilishe malalamiko kwa mamlaka yake ya uteuzi'.

'Vyombo vya dola vichunguze askari wake kuingia studio na kuepusha tukio hilo kujirudia siku za usoni'.

'Clouds ipitie upya miongozo yake na kuzuia watu wanaoingia mara kwa mara chumba cha habari ilhali hawana taaluma ya uhariri'.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)