Kupitia ukurasa wake wa Tweeter Waziri Nape aliandika…>>> ‘Tujifunze kusoma biblia, Nasoma masomo ya Mwakasege watu wanachukua na kutafsiri watakavyo kwa faida zao.Nimesikitishwa sana. Si SAWA!‘
Hii imekuja mara baada ya usiku wa
February 14 2017 kupitia ukurasa wake huohuo Waziri Nape alinukuliwa kwa
kuandika >>>’Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi!‘
Huku akiambatanisha na kipande cha video cha Mchungaji Christopher Mwakasege aliyenukuliwa akisema ‘Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu, sio kwamba hana akili bali amepungukiwa‘
Kwa ufupi ni kwamba Waziri Nape amesema alichokiandika hakijamlenga na wala hajakiweka kwa makusudi yoyote yenye nia ya kumsema kiongozi yeyote, ni utaratibu wake kusoma masomo ya Mwakasege.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni Yako Hapa (Zingatia Maadili)