www.domdaily14.blogspot.com

Tuesday, 21 February 2017

CCM Yamweka Kiporo Yusuf Manji

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, kimesema hakitamjadili Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Yusuph Manji, hadi kesi yake kuhusu madai ya kutumia dawa za kulevya itakapomalizika mahakamani.

Msimamo huo umetolewa baada ya kuwapo  taarifa kwamba

Tundu Lissu: Serikali Ina Hofu Na Mimi TLS

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu, amesema ameanza kuogopwa na viongozi wa serikali  baada ya jina lake kuwa miongoni mwa majina matano bora ya wagombea wa nafasi ya urais katika Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutokana na misimamo yake ya kuitetea Katiba ya Tanzania.

Akizumgumza na waandishi wa habari  Mwanza jana, Lissu alisema  tangu atangaze nia yake ya kugombea urais wa TLS ameanza kuogopwa  kutokana  na kujulikana kwa   misimamo yake kuhusu  masuala ya   sheria,  siasa na  katiba ya nchi hii.

Alisema TLS ina majukumu makubwa katika nchi ya kulinda utawala wa sheria na wanasheria ndiyo wanaojua kuliko mtu yeyote  zinapotungwa sheria mbovu na zile za kikandamizaji, pia wao ndiyo wanapaswa kuwa wa kwanza kuanza kuzipigia kelele sheria hizo.

“Kwa miaka mingi  TLS imeongozwa  na watu ambao hawafikiri kwamba wajibu wao wa kwanza kulinda utawala wa sheria,  wao wanafikiri wajibu wao wa kwanza ni kuwapendeza  wanasiasa na matokeo yake TLS imepotea, wanachoogopa  ni kwamba hii raha ambayo wameipata miaka yote hii wakati  wanasheria wa  TLS wakiwa  usingizini akija huyu Lissu itaisha,” alisema Lissu.

Alisema aligombea nafasi hiyo  baada ya kumsikia Rais Dk. John Magufuli akizungumza mbele  ya watanzania kwamba wakili  yeyote  atakayewatetea  watuhumiwa wanaokutwa na  dawa ya kulevya au nyara za serikali wakamatwe na kuwekwa ndani.

Alisema aliposikia kauli hiyo alicheka na kusema sasa ni wakati wa yeye kuwa rais wa TLS ili kauli za aina hiyo zikome na siku mbili kabla ya Rais Dk. John Magufuli kutoa kauli hiyo,  Bunge lilipitisha sheria ya msaada wa sheria.

“Sheria hiyo inasema mtu yeyote anayefunguliwa kesi ya jinai, au madai kama ni maskini hana uwezo wa kumlipa wakili atapatiwa huduma hiyo na wakili atalipwa  na  mtendaji mkuu wa mahakama.

“Sheria hiyo inampatia haki  mwananchi yeyote atakayekuwa  na kesi ya mauaji, pembe za ndovu au dawa za kulevya  kupata wakili atakayelipwa na serikali.

“Siku mbili baadaye Rais anakinzana na sheria hiyo nilishangaa kweli.  Tayari sheria hiyo imetungwa  ni jambo muhimu kweli kwa sababu katika  nchi hii watu wanasingiziwa sana, kwenye maegereza nyingi   nchini wamejazana wananchi ambao hawana hatia na wapo huko kwa sababu hawakuwa na mawakili wa kuwatetea,” alisema Lissu.

Lissu alisema  endapo atachaguliwa kuwa rais wa TLS atahakikisha sheria ya msaada wa  sheria  inatekelezwa.

Kuhusu hoja ya  Waziri wa katiba na  Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ya kutishia kukifuta chama hicho kwa kuwa kimeanza kujiingiza katika masuala ya siasa, Lissu alisema wanaoleta hoja za kutaka kukifuta chama hicho kama ni wanasheria ujuzi wao wa sheria ni wa shaka lakini kama ni wasiojua sheria wanasamehewa.

Alisema  sheria ya iliyoanzisha TLS inasema mwanachama yeyote aliyekidhi vigezo  vya chama hicho ana haki ya kuwa mgombea wa nafasi yoyote ya uongozi na haijasema  ukiwa mwanachama wa chama chochote cha siasa unapungukiwa sifa  ya kugombea.

“Watu wanazungumza   kana kwamba ni makosa mwanasheria kuwa mwanasiasa, katika nchi hii katiba imeruhusu  siasa za vyama vingi, kuwa wanachamaau  kiongozi wa chama.

“Kuwa tu mwanachama una kuwa na fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini lakini sasa watu wanataka kuaminishwa kuwa ukiwa mwanasiasa huna haki,” alisema

Tuesday, 14 February 2017

Zitto Kabwe Ataka Bunge Livunjwe

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amemshauri Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo analiona ni kikwazo kwake.

Ushauri huo ameutoa jana ikiwa ni saa chache baada ya Rais Magufuli kukosoa uamuzi wa Bunge kumuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kujieleza mbele ya Kamati ya Bunge, kutokana na kilichodaiwa na wabunge kuwa ni kauli

Waziri Nape akerwa na Taarifa zilizosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii kutaka kumgombanisha na baadhi ya Viongozi Wenzake

February 13 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zilizosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodaiwa kutaka kumgombanisha yeye na baadhi ya viongozi wenzake wa serikali.

Friday, 10 February 2017

Anaswa na mzigo wa dawa za kulevya chumbani..... RPC asimulia Sakata Zima

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi  kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha pinchi 240 na ndonga mbili Mkoani

Freeman Mbowe Agoma Kuitikia Wito wa Makonda......Asema Lazima Amshitaki Kwa Kumchafulia Jina


Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji.

Yusuph Manji na Askofu Gwajima Kuendelea Kusota Selo.....Kamanda Sirro Asema Upelelezi Bado Unaendelea

Kamanda Sirro amesema  bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.

Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.

Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .

Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussein Pamba Kali pamoja na bosi wa Sea Cliff.

Friday, 3 February 2017

Mbowe na Naibu Spika Dr Tulia Ndani ya BIFU Jipya

Mvutano  umeibuka bungeni kati ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya Mbunge huyo wa Hai kumwuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa swali lililopingwa na Naibu Spika kwa maelezo kuwa ni la kisheria si la kisera.

Sakata hilo liliibuka asubuhi katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, baada ya Mbowe kuhoji sababu za Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kusota rumande kwa kukosa dhamana, Peter Lijualikali wa Kilombero anayetumikia kifungo cha miezi sita gerezani na wanachama wengine wa Chadema wanaokabiliwa na mashitaka mbalimbali.

Mbowe alimtaka kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni, aeleze kama ni sera ya Serikali kuua vyama vya upinzani, huku akisema Rais John Magufuli alipata kutamka kuwa atavimaliza vyama vya upinzani kabla ya mwaka 2020.

Kwa maswali hayo, Dk Tulia alimtaka Waziri Mkuu kujibu swali linalohusu sera na kuachana na yanayogusa masuala ya kisheria.

Jambo hilo liliwafanya wabunge wa Upinzani huku wakipiga meza kwa takribani dakika tano kupinga, wakimtaka Naibu Spika aache Waziri Mkuu ajibu swali hilo.

Katika swali lake la msingi, Mbowe alisema wakati jana ikiwa ni Siku ya Haki Duniani, imepita miezi mitatu tangu Lema aanze kusota rumande huku akinyimwa dhamana licha ya kuwa iko wazi.

Pia alisema Lijualikali anatumikia kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kisiasa sambamba na mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew aliyefungwa miezi minane na madiwani zaidi ya sita na viongozi wengine 215 nao wakifungwa au kuendelea na mashitaka huku zikifanyika hila za kuidhoofisha CUF.

“Haya yanayoendelea katika Serikali ambayo ni kinyume na utamaduni na mazoea yetu kama Taifa, je ni utekelezaji wa sera ya kuua upinzani chini ya Rais Magufuli?” Alihoji Mbowe.

Kabla ya Waziri Mkuu kujibu swali hilo, Dk Tulia aliingilia kati na hali kuwa hivi:

Dk Tulia: Katika swali lako kuna masuala ya kisera na kisheria. Maswali yanayomhusu Lema na Lijualikali na madiwani sita ni ya kisheria, hayo kuhusu leo (jana) kuwa siku ya haki duniani, Waziri Mkuu anaweza kuyajibu.

Majaliwa: Nakanusha, Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani, nchi inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu na kuna Bunge, Serikali na Mahakama. Hakuna mhimili unaoingilia mhimili mwingine. Jambo lililopo mahakamani halizungumzwi kokote, siwezi kuzungumzia hilo.

Mbowe: Kwa kuwa Rais anaonekana kuvunja Katiba ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, je tukileta ushahidi kuwa Rais amekusudia kuumaliza upinzani kabla ya 2020, Waziri Mkuu utakuwa tayari kuwajibika kwa kujiuzulu?

Dk Tulia: Mbowe swali lako la maelezo ya jumla, yako sawasawa ila la kumtaka Waziri Mkuu kuwajibika si la kisera, kuwajibika si sera uliza swali la kisera.

Mbowe: Labda swali langu nilielekeze kwa Naibu Spika (Dk Tulia). Swali langu lilikuwa la mwendelezo ambalo hutokana na majibu ya msingi yaliyotokea. Kama kulikuwa na msingi wa kisera kwenye swali la msingi, swali la mwendelezo linakwenda kutokana na majibu yaliyotolewa. Waziri Mkuu aseme tu kama yupo tayari kujiuzulu tukileta ushahidi.

Katika maelezo yake, Dk Tulia alitaka Mbowe ajikite katika swali la kisera jambo ambalo Mwenyekiti huyo wa Chadema alipinga na kusisitiza kuwa huenda mambo yanayofanyiwa wapinzani, wabunge, mawaziri Serikali inayafurahia.

Rais Magufuli kateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania anaechukua nafasi ya Mwamunyange

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania kama inavyosomeka kwenye hii taarifa hapa chini.

Aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Davis Mwamunyange ni Venance S. Mabeyo ambapo pamoja na kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Venance anachukua nafasi ya Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu ambapo kitu kingine cha kufahamu ni kwamba Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania, Meja Jenerali James Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance aliyeteuliwa kuwa mkuu wa majeshi.
Uteuzi huu unaanza mara moja ambapo tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadae.

Thursday, 2 February 2017

Mwanamke Atoa Tangazo Gazetini Baada ya Kugundua Mumewe Anachepuka

Mtandao wa TUKO umeripoti kuhusu huyu Mwanamke aliyewaaacha wengi na mshangao baada ya kutumia njia isiyo ya kawaida kumzuia mumewe kuchepuka na kuchukua Mwanamke mwingine.

Mwanamke huyo Mkenya aliyetambulika kwa jina la Wanjiru Kamami ama Shiro alichapisha tangazo kwenye gazeti moja la Kenya akitaka kujuzwa habari na yeyote atakayemwona mumewe akiwa na ‘mpango wa kando’ au Mchepuko.

Katika kitendo cha Mwanamke huyo kuonyesha kwamba yuko serious akaamua kuandika na jina la mume wake pamoja na namba ya simu kwenye hilo tangazo lililosomeka "Hii ni kuwajulisha kwamba huyu aliye kwenye picha ni Mume wa Wanjiru Kamami toka mwaka 1982

"Ukimuona anadanganya Wasichana wa shule, Wanawake wengine au kina mama wa sokoni, mwambie aende nyumbani kwa mke wake au piga simu au sms kwenye 0751 993 571"

Hatua Zilizochukuliwa Na Serikali Dhidi Ya Gazeti La MwanaHalisi Baada Ya Kumuomba Radhi Rais